![]() |
Diamond akiwasili mahakamani hapo. |
MSANII wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ leo amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kusikiliza kesi inayomkabili ya kushindwa kumtunza mtoto wake aliyezaa na msanii mwenzake, Hamisa Mobeto.
![]() |
Diamond na wakili wake mahakamni hapo. |
Katika Shauri la kesi hiyo lililofunguliwa na Hamisa Mobetto akiomba Mahakama iamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto kila mwezi, litaanza kusikiliza leo katika Mahakama ya watoto Kisutu.
![]() |
Mobeto akiwasili mahakamani hapo. |
Akiwa mahakani hapo, Diamond alianza kuchechemea hali iliyoonyesha mguu wake wa kushoto kulikuwa na tatizo ambapo aliekea kwenye gari lake kabla ya kuvua sendozi yake iliyoonekana kuwa imekatika.

Mara baada ya kuwasili katika Mahakama ya Kisutu, Diamond alipitiliza na kuelekea hadi Mahakama ya Watoto iliyopo ndani ya viunga vya Mahakama ya Kisutu ayari kwenda kusikiliza kesi yake hiyo.
No comments:
Post a Comment