Monday, December 18, 2017

KINANA AFUNGUKA NDANI YA MKUTANO MKUU WA CCM.. ANGALIA VIDEO


Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeanza Mkutano wake Mkuu wa Taifa Mjini Dodoma ambapo utafanyika kwa siku mbili, Desemba 18-19, 2017. Mkutano huo  umebeba ajenda kuu ya kukamilisha uchaguzi wa ndani wa chama hicho.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkutano huo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema; "kinachokifanya CCM kuwa imara na kuimarika ni demokrasia ndani ya chama, watu kuwa na uhuru wa kutoa mawazo ndani ya chama."

"Ndani ya CCM, hoja ikijitokeza wanajumbe wana uwezo wa kusema. Tukifika mahali wana-CCM wakaogopa kusema ndani ya vikao, watasema nje ya vikao, na wakisema nje ya vikao, tutakuwa hatarini," alisema Kinana.

Mkutano huo unaoongozwa na Rais John Magufuli umehudhuriwa na viongozi wakuu takribani wote wa CCM wakiwemo marais wastaafu Mzee Ally Hassan Mwinyi na Dkt. Jakaya Kikwete.

No comments: