Tuesday, December 12, 2017

DULLY SYKES ATOKWA POVU KISA BOMBADIER


ETI kisa Bombardier! Mkongwe wa Bongo Fleva nchini, Dully Sykes ametoa povu ikiwemo kutangaza vita na wasanii wa kizazi kipya kwa sababu ya kushindwa kumsapoti kwenye wimbo wake mpya.

Dully Sykes ambaye ameachia wimbo mpya wa Bombardier, alisema wasanii wa sasa ambao wengi ni wapya wana roho mbaya na yeye yuko tayari kupambana nao.

“Wasanii wa sasa wana roho mbaya, hawasapotiani kama wasanii wa zamani, ndiyo maana Bombadier yangu hawajanisaidia kuitangaza, hiyo inaonesha muziki ni vita na mimi niko tayari kupambana nao,” alisema Dully.

No comments: