Tuesday, July 6, 2021

MWANAFUNZI AKUTWA AMEUAWA CHUMBA CHA KUPANGA

Marehemu Emily Chepkemoi enzi za uhai wake.

Mwanafunzi mmoja wa Chuo cha KMTC, Emily Chepkemoi mwenye umri wa miaka 23 amekutwa amefariki kwenye nyumba yake aliyokuwa amepanga huko Oriang Estate, Homabay nchini Kenya huku akiwa na majeraha makubwa.

Polisi baada ya kupata taarifa hiyo wamefika eneo la tukio na kushangazwa na walichokiona kwa binti huyo, hivyo wameanza kufanya uchunguzi wao ili kuweza kupata chanzo.

Emily ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Tiba nchini Kenya ilisemekana amepotea ghafla wala simu yake haipatikani.

Hata hivyo rafiki zake baada ya kuona hivyo waliamua kwenda nyumbani kwake ili wakamsalimie lakini cha ajabu ni kwamba walikuta mwili wa mwanafunzi huyo akiwa amepoteza maisha na akiwa na majeraha mwilini mwake.

Majirani wa mtaa huo pia walishangaa kwani wanadai kuwa toka ameingia ndani mwake Ijumaa hawakumwona akitoka nje, lakini badala yake wakaanza kusikia harufu mbaya kutoka chumbani kwake.


Hata hivyo Dancun Oketch, Mkuu wa Msaidizi wa eneo hilo alisema kuwa mwili wa Emmy ulikuwa na majeraha kadhaa ya kuchomwa na kwamba kifo chake kinasadikika kuwa ni mgogora wa kimapenzi.

Polisi wapo kwenye uchunguzi na kuhakikisha wanampata aliyekuwa mpenzi halisi wa binti huyo pamoja na yule aliyekuwa anachepuka naye ili waweze kujua nani ambaye amehusika katika mauaji hayo.

Wakiongea kwenye tukio hilo huku wakilia, marafiki wa marehemu wamesema kuwa Emmy alikuwa mwema na mwenye moyo mkuu, hivyo hawaelewi chanzo cha kuuwawa kwa rafiki yao na kueleza kuwa wameshangazwa na tukio hilo.

Naye Ochieng Geoffrey alisema, “haki itendeke kwa Emily Chepkemoi ambaye aliuawa nyumbani kwake huko Homabay, kwasababu hilo tukio limewashitua wengi.”

Chanzo: Global Publishers

No comments: