Monday, May 7, 2018

UKATA WAMKWAMISHA CHRISTIAN BELLA

AMA kweli vimekosa grisi! Mkongwe wa Muziki wa Dansi, Christian Bella ‘Obama,’ amesema ukata amemfanya abadili utaratibu wa kufanya shoo zake kwa juma. Amesema Sasa atakuwa anafanya shoo moja badala ya shoo nne hadi tano alizokuwa akifanya awali.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Bella anayebamba na Ngoma ya Shuga alisema kuwa, atakuwa akifanya onesho kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ndani ya Kiwanja cha Mzalendo Pub Kijitonyama Jijini Dar.

“Mashabiki wangu najua wengi mnapenda tufanye makamuziki mara kwa mara lakini kutokana na vyuma kukaza nawaomba tufanye kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ndani ya kiwanja hiki,” alisikika Bella akiwa jukwaani kiwanjani hapo huku akishangiliwa na umati wa mashabiki waliofurika.

No comments: