Wakati wanafunzi wa kidato cha sita nchini wakianza mitihani yao ya taifa leo, mwanafunzi mmoja wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari Kahororo iliyopo katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera amekutwa amejinyonga usiku wa kuamkia jana.
Mkuu wa shule hiyo ya Sekondari Kahororo Mwalimu Omary Ogambaki amemtaja mwanafunzi huyo aliyejinyonga kuwa ni Robert Mabula aliyekuwa anasoma kidato cha sita mchepuo wa CBG na ni mkazi wa wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza.
Aidha amesema kuwa wao wameshangaa sana na hawajajua chanzo cha kifo chake na kuongeza kuwa usiku alikuwa akisoma na wenzie na alikwenda kulala muda wa saa kumi alfajiri kuamkia leo.
Kwa upande wao wanafunzi wa shule hiyo wamesema kuwa kitendo hicho kimewastua sana maana hakuwa na matatizo yoyote na walikuwa wakishirikiana nae kwa upande wa masomo hata usiku wa kuamkia leo walikuwa nae wakati wakijisomea.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Augustine Ollom amesema polisi inaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo maana marehemu hakuacha ujumbe wowote.

No comments:
Post a Comment