Tuesday, May 8, 2018

LORI LA MCHANGA LAPARAMIA BODABODA, LAUA 3 (ANGALIA PICHA)


WATU watatu wamefariki dunia papo hapo na wengine takribani 7 kujeruhiwa vibaya  baada ya kugongwa na lori la mchanga aina ya SCANIA lililodaiwa kupata hitilafu katika mfumo wake wa breki.

Ajali hiyo imetokea katika maeneo ya Boko Magengeni, jana Mei 7, 2018 ambapo inadaiwa lori hilo liliwaparamia watu waliokuwa pembezoni mwa barabara huku likizikanyaga pikipiki kadhaa.

Kufuatia tukio hilo, RPC Kinondoni, Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema bado wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo hasa cha ajali hiyo.

Lori hilo pia liligonga magari mengine ikiwemo Toyota coaster yenye namba T423 CHC ambayo ilikuwa imebeba wanafunzi.

Pia inadaiwa wengine waliojeruhiwa ni wauza mitumba ambao hupanga kando ya barabara huku wengine wengi wakinusurika baada ya kukimbia walipoona ajali.









No comments: