Wednesday, May 2, 2018

FACEBOOK KUONGEZA FARAGHA KWA WATUMIAJI WAKE


Kampuni ya facebook inaongeza faragha kwa watumiaji wake kwa kuweka sehemu ya kufuta historia ya ulichokitafuta katika mtandao huo wa kijamii.

Hivi karibuni kampuni hiyo ilikumbwa na kashfa ya kutothamini faragha za watumiaje wake huku watumiaji zaidi ya millioni hamsini walidukuliwa katika kipindi cha uchaguzi wa Marekani.

Facebook imekua katika sakata la faragha ya watumiaje hivi karibuni, mamilioni ya taarifa za watumiaji zilichukuliwa bila ridhaa na kampuni ya Cambridge Analytical kwa matumizi ya wanasiasa.

Mark Zuckerberg amesema kuwa atahakikisha suala kama hilo halitajitokeza tena, kwa kutengeneza ulinzi zaidi wa mtandao huo.

''Kilichotokea kwa Cambridge Analytica ilikua uvunjifu wa uaminifu wa hali ya juu, walichukua data za watu na kuziuza, hivyo tunatakiwa kuhakikisha kuwa suala hili halitokei tena, kwanza tunaweka vizuizi kwa data ambapo mtu atakua anaombwa kwa ridhaa yake, na pili tunahakikisha tunazijua program mbaya zote zilizo'' alisema Zuckerberg.

Katika mkutano wa mwaka wa kampuni hiyo ya mjini California, Zuckerberg emeongeza pia wanaimarisha faragha ambapo itamruhusu mtumiaji kufuta historia ya kitu alichotafuta.

No comments: