Tuesday, April 24, 2018

MZEE GERALD: NILIGOMBANA NA MWANANGU KISA USANII (VIDEO)


BABA mzazi wa marehemu Agness Gerald ‘Masogange’, Mzee Gerald Waya amefunguka alivyokuwa akigombana na mwanaye huyo akimsihi aachane na mambo ya usanii, kwani mzee huyo alikuwa hayapendi.

Akizungumza mara baada ya mazishi ya mwanaye, Mzee Waya alisema; “Mwanangu alikomea kidato cha pili lakini hata kidato  cha pili hakumaliza kwa sababu ya matatizo. Kuna wakati nilikorofishana naye nikamwambia mimi mambo ya usanii sitaki, akanijibu, ‘sasa baba mimi nitafanya kazi gani wakati unafahamu tangu niko kanisani nilikuwa naimba kwaya?’ Baada ya muda tulikutana tena, tukalimaliza suala hilo, nikamruhusu,” alisema Mzee Gerald.

Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma kilichopo Mwenge jijini Dar ambapo jana aliagwa katika Viwanja vya Leaders na kusafirishwa kwenda kwao Mbeya ambako alizikwa jana Aprili 24, 2018 kijijini kwao Utengule, Mbalizi.

No comments: