ARUSHA. Maandalizi ya mazishi ya Leyla Mtumwa anayedaiwa kuuawa kwa kuchomwa kisu na mumewe, Kema Kasambula nchini Uingereza yanaendelea nyumbani kwao Kaloleni jijini Arusha.
Mwili wa Leyla uliwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jana Aprili 23, 2018 saa 12.00 jioni kutoka Uingereza kwa ndege ya shirika la Qatar na kuhifadhiwa katika hospitali ya Mount Meru ya mkoani Arusha.
Kaka wa marehemu, Abdulmalik Mtumwa amesema kuwa mazishi ya mdogo wake yatafanyika leo mchana.
Leyla aliuawa Machi 30, 2018 kwa kuchomwa kisu aliporejea nyumbani kutoka matembezini usiku.

No comments:
Post a Comment