Tuesday, April 10, 2018

MAGUFULI KUWANIA TUZO YA KIONGOZI BORA AFRIKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania tuzo ya kiongozi bora wa Bara la Afrika, zijulikanazo kwa jina la The African Prestigious Awards zinazotarajia kufanyika nchini Ghana.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Michezo, Sanaa na Utamaduni, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati akimkabidhi bendera msanii wa filamu nchini, Yvonne Cherrie maarufu kwa jina la Monalisa anayetarajia kwenda nchini Ghana katika tuzo hizo ambapo ameweka wazi kwamba Tanzania imepata heshima kubwa katika tuzo hizo zenye heshima kubwa katika bara la Afrika.

Amesema kuwa utendaji kazi uliotukuka wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli na ukuaji wa sekta ya filamu nchini ndiyo vinavochangia kuitangaza nchi katika tuzo za The African Prestigious Awards.

Image result for picha ya monalisa“Tanzania imepata heshima kubwa katika tuzo hizi zenye heshima kubwa katika bara la Afrika ambapo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika, na pia tuna wasanii watatu ndani ya tasnia ya filamu ambao ni King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika,” amesema Dkt. Mwakyembe

Hata hivyo, Monalisa anatarajia kuondoka nchini mapema wiki hii kwenda nchini Ghana kwa ajili ya Tuzo hizo ambapo amewaahidi watanzania kuwa lazima atarudi na tuzo kwani anawawakilisha wasanii wenzake hao wawili pamoja na mpiga picha huyo aliyetajwa na pia aliishukuru serikali kwa kumpatia tiketi kwa ajili ya kufanikisha safari hiyo.

No comments: