Wednesday, April 25, 2018

KOCHA MPYA YANGA AISUBIRI SIMBA KWA HAMU (VIDEO)

Kocha mpya wa Yanga Mkongomani Zahera Mwinyi.

KOCHA mpya wa Yanga Mkongomani Zahera Mwinyi jana mchana alimalizana na uongozi wa Klabu hiyo na kuwaambia mashabiki kwamba anajua vilivyo ugumu na umuhimu wa mechi dhidi ya Simba jumapili ijayo.

Zahera alitua juzi alfajiri ambapo jana alifanya mazungumzo na uongozi na wakakubaliana kwenye mambo mengi ya msingi na leo jumatano asubuhi atatua Morogoro tayari kusalimiana na wachezaji hao na ataangalia mambo kadhaa ndipo arejee Dar es Salaam kusaini mkataba wa Kazi.

Kocha huyo anayezungumza kiswahili kwa lafudhi ya Kikongomani amepewa rasmi nafasi ya George Lwandamina aliyekimbia Yanga na kurudi katika klabu yake ya zamani ya Zesco.


No comments: