Monday, April 23, 2018

GALIS AJITETEA KUZIMIA AKIWA KASHIKILIA KITAMBAA MSIBANI KWA MASOGANGE

Image result for uwoya alivyoshiriki kuaga mwili wa masogange
DAR ES SALAAM.  Baada ya picha yake inayomuonesha kazimia huki akiwa kashikilia kitambaa mkononi kuibua gumzo jana mitandaoni, msanii wa filamu, Rammy Galis ameeleza kuwa hakuwa amezimia ila alijisikia kuishiwa nguvu.

Galis alikuwa mmojawapo wa watu waliobeba jeneza la marehemu Agnes Gerald 'Masogange' katika shughuli za kuuaga mwili zilizofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumatatu Aprili 23, Galis amesema kutokana na kusimama muda mrefu wakati wa shughuli za kuuaga mwili alijikuta akiishiwa nguvu na kuomba msaada kwa wenzie wamuondoe eneo ilipokuwa inafanyikia shughuli hiyo.
Image result for uwoya alivyoshiriki kuaga mwili wa masogange
Galis akiwa na marehemu Agnes Masogange enzi za uhai wake.
"Unajua nilisimama sana tangu tunapofikisha mwili pale viwanjani mpaka watu wanaanza kuaga, nadhani kutokana na hilo nikajikuta naishiwa nguvu, hivyo niliwafahamisha wenzangu kwamba sijisikii vizuri na kuomba waniondoe eneo lile," amesema Galis.

"Hivyo pamoja na wao kuamua kunibeba sio kwamba nilikuwa eti nimepoteza fahamu na ndiyo maana hata kitambaa bado niliweza kukishikilia naomba watu waelewe  hivyo na kuacha kunisema kuwa nilikuwa naigiza siwezi kufanya hivyo katika msiba," amesema msanii huyo aliyewahi kutamba kwenye filamu ya Chausiku.

Mbali ya kucheza filamu ya Hukumu na Masogange enzi za uhai wake, Galis pia alishawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu uliodumu kwa mwaka mmoja (2016-2017).

Masogange alifariki Machi 20 mwaka huu akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo jijini Dar es Salaam, anatarajiwa kuzikwa leo Jumatatu Aprili 23 kijijini kwao Utengule, Mbalizi jijini Mbeya.
Image result for uwoya alivyoshiriki kuaga mwili wa masogange

No comments: