Tuesday, April 10, 2018

WANAWAKE WAENDELEA KUFURIKA OFISINI KWA MAKONDA


DAR ES SALAAM.  Wanawake wenye watoto 'waliotelekezwa' wameanza kumiminika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyeanza kuwasikiliza tangu jana.

Leo asubuhi ya Jumanne Aprili 10, 2018 katika viwanja vya oisi hizo zilizopo Ilala jijini hapa, kumeshuhudiwa akinamama wengi wakiendelea kumiminika hapo ili waweze kupatiwa msaada wa kisheria.

Jana, Makonda alisema baada ya wanawake hao kutoa malalamiko yao, wanaume watafika ofisini kwake kujibu malalamiko ya kutelekeza watoto.

Kutokana na wingi wa wanawake waliojitokeza, Makonda alisema uchukuaji wa malalamiko utafanyika kwa siku tano ikishindikana zitaongezwa na utawekwa utaratibu ili watu wote wapate huduma.

Mmoja wa wanawake hao, Ummy Mohammed Ally alisema, "Amenitelekeza na mtoto na kuniacha katika mazingira magumu.  Ninahangaika na mtoto, sina pa kuishi mpaka sasa.  Nampongeza Makonda kwa kutusaidia na wanaume wanaofanya hivi wawajibishwe," amesema.

"Nimezaa nae akiwa anafanya kazi serikalini, anapokea mshahara zaidi ya milioni 1 ila mimi ananipa Sh.100,000/= tu kwa mwezi.  Tunamuomba hata Rais Magufuli atusikilize akinamama maana ndio tunaoteseka na watoto, wanaume wanatukimbia."

No comments: