Thursday, March 1, 2018

TANZIA: MCHEZAJI WA SIMBA SC AFARIKI DUNIA


Mchezaji wa zamani wa timu ya Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania, Arthur Mambeta amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu jijini Dar es Salaam.

Kutokana na taarifa hizo, Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema wamepokea ujumbe wa kifo cha mchezaji huyo kwa mshtuko mkubwa.  

"Tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa kimataifa wa klabu yetu ya Simba, Arthur Mambeta ambae amefariki jana hapa jijini. Mambeta anakumbukwa sana na wanasimba pale alipotoka kwenye kustaafu soka na kuja kuisaidia klabu yake kuifunga klabu ya Yanga kwenye mchezo wa fainali Ligi kuu goli 1-0. Hiyo ilikuwa mwaka 1973 huko nyuma mchezaji huyo alikuwa ni mshambuliaji mahiri kabla ya kuja kucheza beki," amesema Manara.

Msiba unafanyikia Kigamboni.  Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.

No comments: