Wednesday, March 14, 2018

MWANASAYANSI ALIYETABIRIWA KIFO AKIWA NA MIAKA 20, AFARIKI MIAKA 56 BAADAE


Bad News kwa wanasayansi wote duniani ni kwamba Mwanasayansi mkongwe wa Physics Profesa Stephen Hawkins amefariki dunia asubuhi ya leo March 14, 2018 akiwa na umri wa miaka 76.

Profesa Hawkins ambaye ni Mwingereza na ambaye amefariki akiwa nyumbani kwake Cambridge nchini England, alipimwa na madaktari na kukutwa na ugonjwa wa ‘motor neurone’ mwaka 1962 akiwa na umri wa miaka 20 na kuambiwa amebakiwa na miaka miwili tu ili kufariki kutokana na ugonjwa huo.

Akiwa anaugua ugonjwa huo hadi kifo chake leo, Hawkins aliendelea kufanya kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandika kitabu chake maarufu cha ‘A Brief History of Time’ ambacho kimewahi kuwa moja kati ya vitabu vilivyouzwa zaidi duniani.

Ugonjwa alioupata ulimfanya mwili wake ‘kufa’ taratibu, na akaanza kutumia wheelchair, huku uwezo wake wa kuzungumza ukizidi kupungua siku hata siku, na hata kusikia kwake kukisaidiwa na kifaa maalumu.

Hawkins amewahi kuwa Profesa wa Hesabu katika Chuo Kikuu cha Cambridge. Hawkins na Shahada za Heshima 13 na mwaka 2009, Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama alimtunuku Medali ya Urais ya Uhuru ambayo ni ya heshima ya juu zaidi kwa raia Marekani (the highest civilian honor awarded in America) katika historia.

No comments: