Friday, March 23, 2018

HUKUMU YA BABU SEYA NA PAPII KOCHA KUSOMWA LEO

Kufuatia kesi iliyokuwa inawakabili wasanii wa muziki wa dansi nchini ambao walihukumiwa kifungo cha maisha jela, Papii Kocha na Nguza Viking, Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu (AfCHPR) leo Machi 23, itawasomea hukumu ya kesi yao, kutokana na wawili hao kutofuata taratibu za kisheria mara baada ya kupata msamaha wa Rais.

Mahakama hiyo imefanya maamuzi hayo baada ya kuona wasanii hao hawajaiandika barua ya kuarifu kuwa wamesitisha zoezi la dhamana waliyoiomba pindi walipokuwa wanapinga hukumu yao ya kifungo cha maisha jela  kufuatia kesi iliyokuwa inawakabili ya kunajisi na kulawiti watoto.

Kufuatia hilo Mahakama imesema itaendelea na kazi yake kama kawaida na ikiwa watakutwa na hatia au la kwamba jambo lao limeshapata msamaha na msamaha wa Rais huwezi kuhojiwa popote.

Hayo yamesemwa na Jaji Sylvaine Ore ambaye ni Rais wa AFCHPR, kutoka nchi ya Ivory Cost, ambaye ameahirisha kusoma hukumu hiyo jana, kutokana  na wawili hao kutoonekana mahakamani.
 
"Hakuna mwenye mamlaka ya kuhoji kwa sababu kile kifungo kimeshabatilishwa tayari," amesema Jaji Ore.

Hata hivyo, mwanasheria Daniel Kalasha ametoa maoni yake kuhusiana na hukumu hiyo amesema vyovyote itakavyokuwa hukumu hiyo haiwezi kuathiri msamaha wa Rais waliopata, lakini walipaswa kuitaarifu Mahakama kuachana na kesi hiyo kutokana na sababu hizo.

No comments: