Thursday, March 1, 2018

GIGY MONEY: NIMEKUA NAACHA UTOTO SASA

Gigy Money, siku ya sherehe ya baby shower yake.
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amefunguka kuwa kwa sasa ameachana na mambo ya kitoto ili kuwa mama bora kwa mwanaye anayetarajia kumpata.

Akizungumza na Showbiz Xtra, Gigy alisema kutokana na kwamba anatarajia kupata mtoto hivi karibuni, amejikuta akiachana kabisa na mambo ya kitoto aliyokuwa nayo kabla ya ujauzito na sasa anafikiria mambo ya kiutu uzima zaidi.

“Nimekua kwa kweli, unajua huu ujauzito umenipa funzo la maisha na sasa naenda kuwa mama hivyo ili niwe mama bora lazima nibadilike kwa kila kitu siyo kuendelea na yale maisha ya kitoto ya kujiachia kihasarahasara,” alisema Gigy.

No comments: