Wednesday, March 21, 2018

BOSS WA FACEBOOK AITWA BUNGE LA UINGEREZA KUJIBU TUHUMA

Mkurugenzi na Mwanzilishi wa mtandao maarufu wa Facebook Mark Zuckerberg jana ameitwa kwa barua rasmi na Kamati ya Bunge la nchini Uingereza ili kutoa ushahidi kuhusu kutumia data binafsi za watumiaji wa Facebook kupitia Cambridge Analytica.

Cambridge Analytica  ni kampuni ambayo iko nchini Uingereza ambayo inatuhumiwa kutumia taarifa za wanachama Milioni 50 ili kuweka ushawishi katika Uchaguzi Mkuu wa Urais nchini Marekani uliofanyika mwaka 2016.

Kampuni ya Facebook inatuhumiwa kwa kosa la kushindwa kuwapa taarifa watumiaji wa mtandao huo kuwa, taarifa zao zinaweza kuwa zilipatikana na kutunzwa na kampuni hiyo ya Cambridge Analytica, kampuni ambayo inasemekana kumsaidia Donald Trump kushinda Urais 2016 Marekani.

Hata hivyo Facebook imeeleza kuwa iliifungia kampuni hiyo kupata taarifa za mtandao huo, japokuwa iliweza kupata taarifa hizo kwa njia za udanganyifu na kuvunja sera za mtandao huo.

No comments: