Monday, February 12, 2018

RAIS AMTIMUA KAZI MKUU WA USALAMA

Image result for omar al bashir
Taarifa iliyotolewa na Shirika la habari la Sudan-SUNA iliripoti kwamba Rais wa Sudan Omar al-Bashir amemuondoa madarakani mkuu wake wa usalama na kumrudisha ofisa mwandamizi ambaye alisaidia kuanzisha mashauriano ya usalama na Marekani baada ya mashambulizi ya Septemba 11 yaliyotokea mjini Washington na New York nchini Marekani.

Shirika hilo lilisema Salah Abdallah Mohamed pia anajulikana kama Salah Gosh ambaye alihudumu kama mkuu wa idara ya ujasusi na idara za usalama wa nchi-NISS kati ya mwaka 2004 na 2009 alirudishwa tena kwenye wadhifa huo akichukua nafasi ya Mohammed Atta al-Moula ambaye alihudumu nafasi hiyo tangu mwaka 2009.

No comments: