DAR ES SALAAM. Mtoto mmoja wa kitanzania jana jioni amerudishwa nchini baada wazazi wake kuhukumiwa kifo nchini China kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya.
Wazazi hao ambao ni watanzania, Baraka Malali na mkewe Ashura Mussa
walikamatwa nchini China Januari 19 mwaka huu kwenye uwanja wa ndege wa
Baiyun Guangzhou, wakiwa wamemeza tumboni dawa za kulevya na baada ya kuhifadhiwa
kwenye chumba maalum kwa muda Baraka alitoa pipi 47 kwa njia ya haja
ambapo mkewe alitoa pipi 82.
Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa wameambatana na mtoto wao
wa kike mwenye umri wa miaka 2 na miezi 9. Serikali ya China iliwasiliana na
serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la mtoto huyo ambapo
walikubaliana kumrudisha mtoto huyo nchini ambapo mtoto huyo aliwasili nchini jana saa saba mchana akiwa ameambatana na Afisa wa Wizara
ya Mambo ya Nje ya Nchi, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda.
Serikali kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa
ya Kulevya na Ustawi wa Jamii inafanya jitihada za kuwasiliana na ndugu
na jamaa wa watuhumiwa ili kuhakikisha mtoto huyo anakabidhiwa kwao kwa
ajili ya malezi na matunzo.
Taarifa Na: Rogers W. Siyanga
Kamishna Jenerali:
Mamlaka Ya Kudhibiti Na Kupambana Na Dawa Za Kulevya Nchini
No comments:
Post a Comment