Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka kundi la TMK Wanaume na kiongozi wa Mkubwa na Wanaye Mhe. Temba anadaiwa kumfumania mkewe akiwa na mwanaume na ndiyo chanzo cha kuachana na mkewe huyo, Bibi Cheka ameweka wazi.
Akiongea kwenye kipindi cha eNewz Bibi Cheka amesema kuwa Mhe. Temba alimfumania mkewe akiwa na mwanaume mwingine ndani ya nyumba yake na kumfukuza kisha mwanamke huyo kuolewa na mwanaume mwingine, Bibi Cheka amemwaga mchele huo baada ya kusikia Temba akijitapa kuwa uongozi wao ulimjengea nyumba kubwa na kudai kuwa bibi huyo hana shukrani.
Kwa upande wa Temba alifunguka na kusema kuwa hizo taarifa hazina ukweli wowote kwani yeye na familia yake wapo vizuri wala hakuna jambo kama hilo analodai Bibi Cheka
"Hapana mimi nipo na familia yangu watoto zangu wapo nyumbani na mama yao yupo likizo saizi hivyo nimetoka hapo ameniandalia chai vizuri saizi ndiyo natoka kwenda kuonana na jamaa zangu tuna kikao kidogo, sasa sijui yeye ana ushahidi gani kusema nimeachana na mke wangu na hata kama kweli labda nimeachana naye haihusiani na mambo haya tuzungumze mambo ya muziki, sijawahi kumfumania mke wangu na sijui kwanini bibi amezungumza hayo huenda labda amekasirika," amesema Temba.

No comments:
Post a Comment