Thursday, February 15, 2018

BREAKING NEWS: KIONGOZI WA UPINZANI ZIMBABWE AFARIKI DUNIA

images
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika kusini.
 
Kwa mujibu wa kiongozi Mwandamizi wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC), Tsvangirai mwenye umri wa 65 ameripotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya utumbo.

Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na Makamu Rais wa chama cha MDC, Elias Mudzuri kupitia Shirika la Habari la Uingereza, Reuters kwamba marehemu Tsvangirai alifariki jana jioni, Februar 14.

Morgan Tsvangirai aliyekuwa ni mpinzani mkubwa wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe,  alianzisha chama cha  MDC mwaka 2000, na kuanza kutoa changamoto kwa Rais Mugabe aliyekaa madarakani muda mrefu.

Kufuatia kifo hicho cha Tsvangirai, chama cha MDC kinaweza kugawanyika juu ya nani atakayeongoza uchaguzi hapo baadaye mwaka huu dhini ya chama tawala cha Zanu PF, ambacho kwa sasa kinaongozwa na Emmerson Mnangagwa.

No comments: