* Philison Mdee aongoza kwa wavulana, Ellizabeth Mangu aongoza wasichana
* Wengine 265 matokeo yafutwa, yumo aliyeandika matusi kwenye majibu
* St Francis yashika nafasi ya kwanza.
SHULE ya Sekondari ya St.Francis Girls imeongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2017.
Akitangaza sekondari ambazo zimeshika nafasi za juu kwenye matokeo hayo, leo jijijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde amesema nafasi ya pili imechukuliwa na sekondari ya Feza Boys na nafasi ya tatu sekondari ya Kemebos.
Wakati nafasi ya nne imeshikiliwa na sekondari ya Bethel Saabs Girls, nafasi ya tano sekondari ya Anuarite, nafasi ya sita sekondari ya Marian Gilrs huku nafasi ya saba ikishikiliwa na sekondari ya Canossa, wakati nafasi ya nane imechukuliwa na sekondari ya Feza Girls, nafasi ya tisa sekondari ya Marian Boys na nafasi ya 10 sekondari ya Shamsiye Boys.
WALIOONGOZA 10 BORA KITAIFA
Kwa upande wa wanafunzi ambao wameshika nafasi ya kwanza hadi ya kumi kitaifa kwenye matokeo hayo, Dk.Msonde alisema nafasi ya kwanza imeshikwa na mwanafunzi Philison Mdee (Marian Boys), wakati nafasi ya pili imeshikwa na Eliza Mangu (Marian Girls), nafasi ya tatu Anna Mshana (Marian Girls).
Ametaja nafasi ya nne imeshikwa na Emanuel Makoye (Ilboru), nafasi ya tano Lukelo Luoga (Ilboru), nafasi ya sita Fuad Thabit (Feza Boys), nafasi ya saba Godfrey Mwakatage (Uwata), nafasi ya nane Baraka Mohamed (Angeles), nafasi ya tisa Lilian Moses (Marian Girls) na nafasi ya kumi kitaifa imechukuliwa na Everine Mlowe (St. Francis Gr)
WAVULANA 10 BORA KITAIFA
Akitangaza walioshika nafasi ya kwanza hadi ya 10 kitaifa kwa mujibu wa Dk. Msonde ni Philison Mdee (Marian Boys), nafasi ya pili Lameck Makoye (Ilboru), nafasi ya tatu Tadei Luoga (Ilboru), nafasi ya nne Fuad Thabit (Feza Boys).
Wakati nafasi ya tano ni Godfrey Mwakatage (Uwata),nafasi ya sita Baraka Mohamed (Angeles),nafasi ya saba Noel Shimba (Marian Boys), nafasi ya nane ni Patrick Robert (Mzumbe), nafasi ya tisa Robison Eliona (Ilboru) na nafasi ya 10 bora kitaifa imechukuliwa na mwanafunzi Harrison Simkoko (Mzumbe).

No comments:
Post a Comment