Friday, December 15, 2017

SABABU ZA KUAHIRISHWA MNADA WA NYUMBA ZA LUGUMI, MOJA YANUNULIWA NA MTANZANIA


Tarehe 14 Desemba, 2017 kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart ya jijini Dar es Salaam ambayo inasimamia mnada wa kuuza nyumba tatu za kifahari mali ya Lugumi Enterprises  Ltd, imetangaza kuahirisha mnada wa nyumba hizo mpaka watakapotangaza tena.

Akiongea na vyombo vya habari, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Scolastica Kivela ameeleza sababu zilizosababisha mnada wa nyumba mbili kati ya tatu kuahirishwa na kusema kuwa moja tayari imenunuliwa.

“Leo tumewaita ili tuongelee kuhusu kuahirishwa kwa mnada wa nyumba mbili za Lugumi, natangaza mnada huu umeahirishwa mpaka tutakapotangaza tena. Plot moja ya Mbweni JKT imenunuliwa; mwenzetu mmoja Mtanzania aishie nchini Uingereza amejipatia nyumba ile,”  amesema Scolastica.


No comments: