![]() |
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Rais Dkt Ali Mohamed Shein akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Kheri James mara baada ya kushinda katika uchaguzi wa jumuiya hiyo uliofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Chuo Cha Mipango mjini Dodoma. Wa pili kulia anayeangalia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Bi. Tabia Mwita. |
![]() |
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Rais Dkt Ali Mohamed Shein (kushoto) akimpongeza Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Bi. Tabia Mwita baada ya ushindi wake. Katikati anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. |
![]() |
Mara baada ya kutangazwa tu kuwa ndiye Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya umoja wa Vijana (UVCCM), Kheri Denis James, kwa furaha kubwa iliyokwenda mpaka kwa Wajumbe wenzake,ilibidi zitumike nguvu za ziada kupunguza vurugu za shangwe zilizotarajiwa kutokea ukumbini hapo, kama uonavyo Mwenyekiti akiwa katika mikono salama ya utulivu akielekezwa kwenda jukwaa kuu. |
![]() |
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu na Mkutano mkuu wa UVCCM wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi katika mkutano huo. |
![]() |
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake Mh. Mboni Mhita akimpongeza Makamu Mwenyekiti mpya Bi. Tabia Mwita. |
![]() |
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Mh. Kassim Majaliwa pichani kushoto akitazama tukio la pongezi kutoka Makamu Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake Mh. Mboni Mhita akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Kheri James. |
No comments:
Post a Comment