Friday, November 24, 2017

BREAKING NEWS: OFISI YA MTENDAJI UBUNGO YATEKETEA KWA MOTO

Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Saranga, Ubungo, jijini Dar es Salaam,  imeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo, huku baadhi ya mali na nyaraka za serikali zilizokuwemo zikiteketea.

Kwa mujibu wa wahusika, chanzo  cha moto huo hakijajulikana lakini juhudi zinaendelea kumpata Mtendaji wa kata hiyo ili kujua hasara iliyotokana na moto huo na ni vitu au mali gani zilizokuwemo katika ofisi hiyo.
Viongozi wa Serikali za Mtaa wakikagua uharibifu uliotokana na moto huo.

Muonekanao wa ndani wa ofisi hiyo.

No comments: