Wednesday, November 15, 2017

BREAKING NEWS: ALIYEKUWA MUME WA IRENE UWOYA, HAMAD NDIKUMANA AFARIKI GHAFLA

Marehemu Hamad Ndikumana, enzi za uhai wake.
ALIYEKUWA mume wa muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya, mchezaji mpira wa miguu Hamad Ndikumana 'Kataut' (39) kutoka nchini Rwanda amefariki usiku wa kuamkia leo nchini humo huku chanzo cha kifo chake kikisemekana kuwa ni kuugua ghafla.
 

Taarifa kutoka Kigali, Rwanda zinaeleza Kataut alikuwa mazoezini jana asubuhi.

Wakati anapoteza maisha, Kataut alikuwa kocha msaidizi wa kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda.

Mara ya mwisho, Kataut aliichezea Stand United ya Shinyanga wakati akitokea Cyprus.

Alikuja nchini mara ya mwisho wakati wa Simba Day Agosti 8, akitua nchini Agosti 7 akiwa na kikosi cha Rayon ambacho kilicheza na Simba na kupoteza kwa bao 1-0.


Marehemu Ndikumana alizaliwa Oktoba 5, 1978 na mpaka anafariki dunia alikuwa ametengana na mkewe huyo kwa miaka kadhaa.  Wawili hao walifunga ndoa katika Kanisa Katoliki la St. Joseph la jijini Dar es Salaam mwaka 2009 na walibahatika kupata mtoto mmoja  wa kiume aitwaye Krish.

Picha kadha za harusi yao:
[2.JPG]

Baadhi ya posti za mwisho marehemu Ndikumana:





Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Hamad Ndikumana, Amen.

No comments: