Tuesday, October 31, 2017

ZITTO KABWE AKAMATWA NA POLISI

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa asubuhi hii na Afisa Habari wa Chama cha ACT, Bwana Abdallah Khamis imeeleza kuwa KIONGOZI wa Chama hicho, Zitto Kabwe, amekamatwa na jeshi la Polisi leo asubuhi akiwa nyumbani kwake na amepelekwa kituo cha Polisi Chang'ombe.

Sababu za kukamatwa kwake ni hotuba ya juzi Oktoba 29, 2017 katika kata ya Kijichi, Mbagala Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani kwenye kata 43 nchini.

No comments: