Sophia Biambina mmoja kati ya watu watatu walionusurika kwenye ajali ya daladala aina ya Hiace iliyotumbukia Ziwa Victoria katika eneo la Kigongo wilayani Misungwi akiwa amelazwa katika Hospitali ya Bukumbi Mission iliyopo wilani humomkoani Mwanza jana. Watoto wawili wa Sophia wamepoteza maisha katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 12. Picha na Johari Shani |
Hii unaweza kuiita simulizi iliyojaa uchungu mwingi kwa Sophia Biambina (32) ambaye ni mmoja wa watu wachache walionusurika katika ajali ya basi lililozama katika Ziwa Victoria juzi.
Mama huyo ambaye alipoteza watoto wawili wakati basi hilo aina ya Toyota Hiace lilipotumbukia katika eneo la Kigongo Feri wilayani Misungwi, Mwanza, alikuwa akirejea nyumbani kwake Nyapande, Sengerema akitokea Magu kwenye msiba wa baba yake.
“Baada ya ajali nilijikuta nimeshatoka nje sikujua nimetokaje, najihisi maumivu makali kwa sababu nilikunywa maji mengi. Kinachoniuma ni kuwapoteza watoto wangu, tulitoka msibani kumzika baba yangu,” alisema.
Majeruhi mwingine, aliyezungumza akiwa katika Hospitali ya Bukumbi Mission wilayani Misungwi alikolazwa, Yohana Ngabula (28) mkazi wa Kijiji cha Buyagu, Sengerema naye alisema amepoteza mama na dada katika ajali hiyo.
Ngabula alisimulia kwamba nao walikuwa wakitokea jijini Mwanza kufuatilia mafao ya baba yao katika ofisi za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
“Nilimshauri dereva agonge hata gari lililokuwa mbele yake badala ya kulielekeza ziwani lakini hakusikia mwisho wake ndiyo hayo yaliyotokea,” alisema na kuongeza kuwa baada ya gari kutumbukia ziwani alipasua kioo na kutoka ndipo walipofika vijana wakamuokoa.
Majeruhi mwingine mkazi wa Ibisabageni, Paulo Lazaro ambaye ni mwalimu wilayani Sengerema naye anakumbuka jinsi walivyomshauri dereva huyo, “Tulimshauri agonge vitu nchi kavu kuliko kuipeleka gari majini lakini hakusikiliza ushauri wetu, pengine tungepona wengi zaidi.”
Mwalimu huyo ambaye aliumia bega na mgongo alisema alipita dirishani baada ya gari kutumbukia ziwani.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Bukumbi, Dk Robert Shija alisema walipokea maiti 12 na majeruhi hao watatu.
Aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Joseph Paulo, Rehema Makalanga, Mariamu Kagosha, Pendo Msafiri, Salome Msafiri, Joyce Hamadi, Martha Makenzi, Gwanchele Mswagi na Kazungu Lukuba wote wakazi wa Wilaya ya Sengerema. Wengine ni Martine Kamlamo mkazi wa Bukumbi, Hamadi Zahalaki wa Bukoba na Ally Abdul wa Kayenze wilayani Ilemela.
Ili kuhakikisha wote waliofariki dunia wanazikwa kwa heshima zote, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda ameuagiza uongozi wa hospitali kuwa, ndugu watakaoshindwa kusafirisha miili wawasiliane na ofisi ya wilaya kwa ajili ya msaada.
Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole alisema walipanga kuisafirisha miili hiyo lakini tayari ndugu wameshaichukua.

No comments:
Post a Comment