Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda
amesema ameguswa na hisia za Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),
Tundu Lissu.
Ponda amesema hayo leo alipokuwa akizungumzia safari yake ya Nairobi nchini Kenya alikokwenda kumjulia hali Lissu hivi karibuni.
“Tulipokuwa tunabadilishana mawazo, niliguswa na hisia kubwa, badala ya
mimi kumpa matumaini yeye ndiye alinipa matumaini,” amesema Ponda.
Amesema madhumuni ya safari yake yalikuwa kumjulia hali Lissu,
kumwombea dua, kumjengea matumaini ya afya na kujenga mazingira mapana
yanayotosha kulizungumza jambo lililomfika.
No comments:
Post a Comment