 |
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Seleman Said Jafo akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amewaapisha Mawaziri 8 na Manaibu Waziri 16, aliowateua, baada ya kufanya mabadiliko ya Baraza hilo Oktoba 7, 2017.
Sherehe za kuapishwa kwao zimefanyika Ikulu jijini Dar es salaam, na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kitaifa, wakiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma.
Baada ya kuapishwa Rais Magufuli amewataka Mawaziri hao kuanza kazi mara moja, na wamebadilishana nyaraka mbali mbali za wizara ambazo walikuwa wanatumikia awali, kwa wale ambao wamehamishwa wizara.
 |
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Daniel Shonza akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. |
 |
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Justus Nditiye akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. |
 |
Waziri wa Madini Mhe Angellah Jasmine Kairuki akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. |
No comments:
Post a Comment