Monday, October 2, 2017

BREAKING NEWS: WATU 50 WAUAWA KATIKA TAMASHA LA MUZIKI LAS VEGAS, MAREKANI

People fleeing from scene of country music festival
Zaidi ya watu 50 wameuawa na takriban 200 kujeruhiwa kwenye ufyatuaji wa risasi wakati wa tamasha la muziki huko Las Vegas, Marekani.

Mtu mwenye bunduki mwenye umri wa miaka 64 Stephen Paddock alifyatua risasi kutoka ghorofa ya 32 kwenye hoteli ya Mandalay Bay, kwenda kwenye tamasha lililokuwa likiendelea nje.

Polisi wanasema mshukiwa ambaye alitajwa kuwa mkaazi wa mji huo na ambaye hakutajwa jina ameuawa.

Mamia ya watu walikimbia eneo hilo na milio ya risasi ikasikika kwa muda kwenye video zilizochapishwa katika mitandao ya kijamii.
Chanzo: BBC Swahili
Eneo la mauaji

No comments: