Mkuu wa Polisi nchini (IGP) Simon Sirro amesema Jeshi lake linaendelea na upelelezi juu ya taarifa za mwanaharakati wa mitandao ya kijamii anayeishi Marekani, Mange Kimambi, kuwakejeli na kuwatukana viongozi wa nchi kwenye mitandao.
Akizungumza na wanahabari katika ofisi za Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Sirro alisema "Kwenye kazi hii ya upelelezi huwezi kuwaka kila kitu wazi, tunajua (Mange) anavunja sheria za nchi, tunafanya nini, siwezi kusema," alisema.
Sirro ametoa msimamo huo baada ya hizi karibuni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema hawatavumilia vitendo vinavyofanywa na Kimambi pamoja na kundi lake.
Katika taarifa hiyo Boaz alisema jeshi hilo litawasaka na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola watu wanaoshirikiana na mwanaharakati huyo kutoa taarifa za uongo, uzushi, matusi na kejeli kwa viongozi wa nchi.
Kamanda Sirro alikuwa mjini Iringa jana katika mwendelezo wa ziara zake za kufanya ukaguzi wa jeshi hilo na kuzungumza na maafisa wa Polisi, askari na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mikoa mbalimbali.

No comments:
Post a Comment