Wednesday, October 4, 2017

MKOSOAJI WA KAGAME AFUNGULIWA MASHTAKA YA KUCHOCHERA UASI

Diane Rwigara
Bi Diane Rwigara.
Mkosoaji mkubwa wa Rais wa Rwanda Paul Kagame, Diane Rwigara ameshtakiwa kwa kuchochea uasi dhidi ya serikali.

Ameshtakiwa pamoja na mama yake Adeline Rwigara na dada yake Anne Rwigara.

Diane Rwigara alizuiwa kuwania urais wa mwezi Agosti mwaka huu nchini Rwanda.

Rais wa sasa Paul Kahame alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 99, na kupelekea madai kuwa kulikuwa na udanganyifu, madai ambayo yalipingwa na mamlaka ya nchi hiyo.

Diane Rwigara pia ameshtakiwa kwa kubuni stakabadhi bandia.

Wachunguzi wanadai kuwa Bi Rwigara alivunja sheria za uchaguzi kwa kukusanya saini bandia kuunga mkono ugombeaji wake.

Haijulikani ni kitu gani kilichangia afunguliwe mashtaka ya kuchochea uasi.
Chanzo:BBC Swahili

No comments: