Bi Miriam Mrita (katikati). |
WAKILI wa utetezi katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Msuya, Miriam Mrita (41) na mfanyabiashara Revocatus Muyela (40), ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumuita Afisa wa upelelezi makosa ya jinai wa Temeke,(RCO) aje aeleze upelelezi wa kesi hiyo umefikia wapi.
Wakili Peter Kibatala amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba baada ya wakili wa Serikali Estazia Wilson kudai kesi hiyo leo ilikuja kwaajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.
Hakimu Simba amekubaliana na ombi hilo la upande wa utetezi na kusisistiza kuwa RCO aitwe mahakamani hapo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 16 Oktoba 2017 kwa ajili ya kutajwa.
Februari 23, mwaka huu, washtakiwa hao waliachiwa huru na Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kisha wakakamatwa tena na baadaye kusomewa mashtaka hayo ya mauaji upya.
Katika kesi hiyo namba 5/2017 inadaiwa Mei 25, mwaka jana maeneo ya Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam, kwa makusudi washtakiwa walimuua dada wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya.

![]() |
Miriam Mrita, mke wa marehemu Bilionea Msuya (katikati) akiwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, DSM leo. |
No comments:
Post a Comment