Jumla wa watu 12 wamekufa na watatu wameokolewa wakiwa salama baada ya Toyota Hiace kutumbukia Ziwa Victoria katika kivuko cha Kigongo Feri wilayani Misungwi.
“Kwa sasa uokoaji unaendelea, abiria wawili ndio wametoka salama. Maiti nane zimeopolewa,” amesema Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) Mkoa wa Mwanza, Ferdinand Mshama ambao ndio wasimamizi wa kivuko hicho.
Mshama akizungumza leo Jumatatu amesema gari hilo linafanya safari kati ya Buhongwa jijini Mwanza na kivukoni hapo.
Amesema ajali hiyo imetokea kutokana na gari hilo kupata hitilafu kwenye mfumo wa breki hivyo liligonga geti la kivuko na kutumbukia ziwani.
“Ni kweli gari limetumbukia, lilikuwa likitokea Buhongwa kupeleka abiria kivukoni, kabla dereva hajapaki lilifeli breki,” amesema na kwamba dereva alipita upande wa magari makubwa.

Hata hivyo, taarifa zilizopatikana baadaye zinasema maiti nne zaidi zilipatikana pamoja na mtu mwingine mmoja kuokolewa na kufanya jumla ya waliofariki kufikia 12 na majeruhi watatu.
Mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu na kuwajalia uponyaji wa haraka majeruhi wote.

No comments:
Post a Comment