Ajali mbaya iliyohusisha magari mawili, Lori na Basi ndogo aina ya Toyota Coaster, imetokea karibu na mto Katonga, barabara ya Masaka huko Kampala, Uganda, usiku wa kuamkia jana Septemba 18, 2017.
Jumla ya abiria waliokuwa kwenye gari ni abiria 19. Kati yao 13 wamefariki dunia na 6 wamelazwa Nsambya hospital.
Basi hilo dogo lilikuwa likiwarudisha Watanzania wa Familia ya Bw Gregory Teu ambao walikwenda kwenye harusi tarehe 16/09/2017 huko Kampala. Bibi harusi ni mtoto wa Bw na Bibi Gregory Teu wa Dar es Salaam.
Ubalozi unaendelea kufuatilia msiba huu pamoja na kupata majina yote ya waliokufa na kunusurika.
Naibu Balozi Mhe. Maleko pamoja na Brigedia Generali S Makona wameelekea Nsambya Hospital kuona walionusurika.

![]() |
Lori na Basi ndogo aina ya Toyota Coaster yaliyohusika kwenye ajali hiyo. |
![]() |
Majina yaliyopatikana kufuatia ajali hiyo. |
MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI NA KUWAPA UPONYAJI WA HARAKA MAJERUHI WOTE!!
No comments:
Post a Comment