Wednesday, September 20, 2017

MIILI YA WATANZANIA 13 WALIOFARIKI AJALINI UGANDA YAWASILI

Watu 13 wa familia moja waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea Uganda baada ya basi walilokuwa wanasafiria kutoka kwenye sherehe ya harusi kugongana na lori imefikishwa Tanzania na kupokelewa jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam (JNIA).

Miili hiyo imepokelewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kupelekwa moja kwa moja katika Hospitali ya Lugalo na inatarajiwa kuagwa leo.

Watu hao walipata ajali tarehe 17 Septemba, 2017 majira ya saa 4:00 usiku katika barabara ya Masaka, Uganda wakiwa njiani kurejea Tanzania wakiwa ni kutoka katika familia ya Naibu Waziri na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mpwapwa, Dodoma, Gregory Teu.

Angalia video ya ndege hiyo ikiwasili JNIA jana usiku:


No comments: