DSM. Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamemjeruhi kwa risasi Meja Jenerali mstaafu, Vincent Mritaba na kumpora Shilingi milioni 5.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa Meja Jenerali Mritaba alipita risasi jana Jumatatu jioni nje ya nyumba yake Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Amesema Meja Jenerali Mritaba alifikwa na mkasa huo akitoka kuchukua fedha hizo katika benki ya NMB tawi la Tangi Bovu.
"Vijana waliokuwa na bodaboda walikuwa wakimfuatilia muda mrefu na alipofika getini walimfyatulia risasi na kumjeruhi tumboni na bega la kulia," amesema Kamanda Mambosasa.
Kamanda Mambosasa amesema kuwa Meja Jenerali Mritaba amelazwa katika hospitali ya Jehsi ya Lugalo ambako anaendelea na matibabu.

No comments:
Post a Comment