Tuesday, September 19, 2017

MANJI AFIKA TENA MAHAKAMANI SIKU 4 TANGU KUACHIWA HURU


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inatarajia kusikiliza kwa siku tatu mfululizo ushahidi wa utetezi katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Mfanyabiashara Yusuf Manji kuanzia September 25 hadi 27, 2017.

Wakili wa Serikali Mkuu, Timony Vitalis amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa, kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini yeye ana safari akidai kuwa jana mchana anataka kusafiri, hivyo ushahidi wa kesi hiyo ukianza kusikilizwa atachelewa.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mkeha alimuuliza Manji kwa nini amechelewa kufika Mahakamani, ambapo Manji alijibu alikuwa eneo la karibu hivyo alisubiri aitwe na Wakili wake.

”Nisamehe sana Mheshimiwa, niliambiwa umetoka, hivyo nilisubiri Wakili anipigie simu kama ungerudi…”

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hiyo hadi September 25-27, 2017 kwa ajili ya kusikilizwa mfululizo.

No comments: