Friday, September 8, 2017

MAGHOROFA YA LUGUMI KUPIGWA MNADA KESHO

Nyumba iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam
Mojawapo ya nyumba za kampuni ya Lugumi Enterprises iliyopo Upanga mtaa wa Mazengo jijini Dar es Salaam ambayo inategemewa kupigwa mnada kesho na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart.
DAR ES SALAAM.  Kampuni ya Udalali ya Yono kesho itapiga mnada maghorofa mawili yanayomilikiwa na kampuni ya Lugumi.

Maghorofa hayo yapo sehemu tofauti jijini Dar es Salaam, moja likiwa mtaa wa Mazengo, Upanga na lingine likiwa Mbweni.

Mkurugenzi wa Yono, Scholastica Kevela amesema leo Ijumaa kuwa wametumia njia mbalimbali ili kufanikisha mnada huo hasa kwa kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Amesema hawezi kutaja gharama halisi ya mali hizo na deni ambalo kampuni hiyo inadaiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) na kwamba TRA wenyewe ndio wanaoweza kutoa majibu hayo.

"Kazi yetu sisi ni kupiga mnada tu, gharama ya deni na thamani ya mali hizo TRA ndio wanatakiwa kutolea majibu," amesema Kevela.

Amesema fedha watakazozipata zitakwenda kusaidia nchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

No comments: