Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtia hatiani aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) David Mataka na aliyekuwa Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha ambaye ni Askofu wa Kanisa la Pentecoste Motomoto, Elisaph Mathew.
Wawili hao wamehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela ama kulipa faini ya Sh.milioni 70 ambapo Hakimu Mkazi Mkuu Victoria Nongwa, pia ameamuru watu hao kulipa hasara waliyoisababishia ATCL katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo gharama yake ni zaidi ya milioni 300 za Kitanzania.
Aidha mahakama hiyo imemuachia huru aliekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za ndani wa ATCL, William Haji.
Wawili hao wamehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela ama kulipa faini ya Sh.milioni 70 ambapo Hakimu Mkazi Mkuu Victoria Nongwa, pia ameamuru watu hao kulipa hasara waliyoisababishia ATCL katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo gharama yake ni zaidi ya milioni 300 za Kitanzania.

No comments:
Post a Comment