Friday, May 22, 2015

STEVE NYERERE AJIBU SHUTUMA YA KULA HELA ZA KUJENGEA KABURI LA MAREHEMU ADAM KUAMBIANA

Msanii Steven Mengere a.k.a. Steve Nyerere.

PhotoGrid_1432293123090
Baadhi ya magazeti yaliyoandika kuhusu shutuma hizo.

Na Ipyana Mwaipaja

Kufuatia magazeti pendwa kadhaa kumuandika staa wa bongo movie, Steven Mengere "Steve Nyerere" kuwa amekula hela za kujengea kaburi la marehemu Adam Kuambiana, Steve amejitokeza leo na kukanusha shutuma hizo.
Akizungumza kupitia redio ya Clouds katika kipindi cha Leo Tena, Steve ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa Bongo Movie,  amekanusha kuwa shutuma hizo si za kweli na kwamba zina lengo la kumchafua tu.

Akielezea kusikitishwa kwake na shutuma hizo, Steve pia ameapa kutojihusisha na masuala ya matatizo ya wasanii tena kutokana na kuchoshwa na kuzushiwa tuhuma za uongo kila mara kuhusiana na masuala ya fedha.

"Kwa kweli nimechoshwa na kila siku watu kunigeuza jalala, kunizushia maneno ya uongo na  kuanzia leo sitaki msanii yoyote anihusishe na masuala kama haya. " amesema Steve.

Katika kipindi hicho, Steve amepambanishwa na msanii Kulwa Kikumba (Dude) ambaye kupitia mtandao wa jamii wa Instagram wawili hao walirushiana maneno ya kulaumiana kuhusiana na  kuzuka kwa kashfa hiyo.  
 
Katika mjadala huo Dude amethibitisha kwamba hakumtuhumu Steve na kwamba yeye hakuandika lolote baya katika mtandao wowote wa kijamii kuhusiana na Steve na sakata hilo.

Hata hivyo, Steve amesema kuwa alitumia ubinadamu kuomba michango ili na wao kama wasanii wawe wameshiriki katika ujenzi wa kaburi hilo na siyo kumuachia mke wa marehemu pekee na kwamba hela hizo hazikupitia mikononi mwake bali zilishikwa na mtu aliyemtaja kwa jina la Danny Nyalusi ambaye ndiye aliyemkabidhi mke wa marehemu pesa hizo. 

"Kwa jitihada zangu nilifanikiwa kupata pesa taslimu Sh. milioni moja ambazo Sh. laki tatu zilitoka kwa msanii Jacob Stevens (JB) na laki saba kutoka kwa mheshimiwa Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na pesa zote ziliwasilishwa kwa mhusika ambaye ni mke wa marehemu" amesema Steve.

Baada ya wawili hao kuwekwa sawa na waendesha kipindi Husna Abdul, Mussa Hussein na Geah Habib, hatimaye wote wawili walikubaliana kuwa yameisha na kuishia kuwalaumu waandishi wa habari kwa kuandika habari bila kuhakikisha wanapata ukweli wa suala zima kutoka kwa wahusika.

BATULI: KANUMBA KAMA KAACHA LAANA KWENYE FILAMU ZA BONGO





 
APRILI 7 mwaka 2012 tasnia ya filamu ilipatwa na majonzi makubwa kutokana na kifo cha aliyekuwa mwigizaji nguli, Steven Kanumba, ambaye alikuwa kipenzi cha wengi ndani na nje ya nchi.

Licha ya wengi kutokuamini kwa muda huo, baada ya muda ikagundulika kweli amefariki, hivyo majonzi zaidi yakarindima, huku kila mtu akisema lake kuhusu kifo hicho.

Baada ya mazishi yake mashabiki walijipa matumaini kwamba tasnia hiyo licha ya kumpoteza mwigizaji huyo ingeendelea vema kutokana na kuwa na idadi kubwa ya waigizaji wenye sifa kama za Kanumba, lakini hadi leo mwaka wa tatu tasnia hiyo inaonekana kupoteza mvuto.

Mwigizaji, Yobnesh Yussuf ‘Batuli’, alipotembelea Kampuni ya New Habari (2006) Ltd , aliongeza chachu ya kutaka kujua zaidi anamkumbukaje Kanumba ambaye waliwahi kufanya kazi kwa ukaribu.

“Wasanii wengi hatujui tatizo ni nini, ndiyo maana naweza kusema kama ameacha laana kwa kuwa tumekutana mara kwa mara kuzungumzia jambo hilo, lakini kama tumeshindwa tumejitahidi na hakuna aliyeweza kufikia mvuto na uwezo wake kwa mashabiki, ndiyo maana tunaonekana kama tunapoteza mwelekeo na kifo chake ni kama kimeacha laana kwa filamu za Tanzania,’’ anaeleza Batuli.

Batuli, mwenye watoto wawili ambaye amezaa mapema kwa hofu ya uzuri wake kuisha kabla ya kupata motto, anasema wakati mwingine wanajikuta wakisema kwamba kwa sasa wanasubiri muujiza ya Mungu ndiyo kutokee mapinduzi mapya katika filamu za bongo, maana kwa sasa hali imeyumba.

Tatizo nini?
Batuli anasema zipo changamoto nyingi zinazowafanya wasifikie mafanikio aliyokuwa nayo Kanumba katika filamu, likiwemo la kutokuaminiwa na wafadhili kunakotokana na baadhi ya waigizaji maarufu wenye majina makubwa katika tasnia hiyo kudhulumu wafadhili hao kiasi kwamba hawataki kufanya kazi na waigizaji wengine wa filamu.

“Wapo wafadhili wameshatoa fedha nyingi kwa baadhi ya masupastaa wetu ili watengeneze filamu zenye ubora na kiwango cha juu ili kuleta hamasa katika soko la filamu kama ilivyokuwa enzi za Kanumba, lakini hakuna aliyethubutu hadi leo, wengi wao wametumia kwa maslahi ya pombe, mapenzi na mambo mengine, wamesahau kwamba walipewa fedha kwa ajili ya kufanyia mapinduzi ya filamu,’’ anaeleza.

Licha ya hayo, Batuli bado anaamini kwamba Kanumba alikuwa na vitu vingi vya ziada vilivyomfanya apendwe ndani na nje ya nchi, vikiwemo uthubutu wake, kujitambua na kuwa na uchungu wa mafanikio.

“Kanumba alikuwa hakurupuki, alikuwa hakati tamaa, hata alipokuwa akichekwa aliamini ipo siku atapigiwa vigelegele, alikuwa mbunifu na mpenda kukosolewa asiye na woga wa kufanya lolote analoona ni fursa kwake,’’ anaendelea kumuelezea.

Anasema: “Kuna kipindi alikuwa anajipanga kwenda kuigiza na waigizaji wa Nigeria, aliponiambia mpango wake huo nilicheka kwamba anakwenda huko ataongea Kiingereza gani, lakini sikuamini jibu lake alisema watajua huko huko, kweli alikwenda na akaigiza na waigizaji wa Nigeria ambao ni maarufu.

“Nakumbuka tulikuwa tukikutana naye kwenye masomo ya Kiingereza, alipokwenda Big Brother watu walicheka Kiingereza chake, lakini hakukata tama, alizidi kujifunza na kujituma, hatimaye akacheza filamu ya “Moses” na mwigizaji maarufu nchini Nigeria, Ramsey Noah, tena kwa Kiingereza kizuri, kila mmoja akaikubali filamu hiyo na ujio wake wa kutangaza soko kimataifa,’’ anaeleza Batuli huku akidai kwamba ni vigumu kuziba pengo la Kanumba.

Haki miliki
Akizungumzia haki miliki, Batuli anaeleza kwamba ni jambo baya linalowaumiza wasanii kwa kuwa baadhi ya wasambazaji wananunua hakimiliki za wasanii, hivyo wakifariki dunia hukosa haki zao nyingi za msingi.

“Mfano mzuri ni kwa Kanumba, kama kungekuwa na hakimiliki ya kazi zake nadhani filamu zake zingeendelea kuuzwa na fedha zingesaidia familia yake, lakini nadhani kwa sasa hali si hivyo, ushauri wangu ni kwamba wanunuaji wa kazi za wasanii wasinunue hakimiliki za kazi zao ili wawasaidie kupiga hatua ya kimaendeleo,’’ anaeleza.

Mapenzi
Batuli anasema alikuwa anafahamu kwamba mwigizaji mwenzake, Nice Mohamed ‘Mtunisi’ alikuwa akimpenda muda mrefu lakini alikuwa mzito kumtamkia.

“Mtunisi aliniogopa, domo zege, wajanja walimuwahi lakini baada ya kusikia nimeachana na mume wangu wa mwanzo akaja kwa gia zote, nikamkubali tukawa wapenzi, lakini hatukupata mtoto,” anaeleza.

“Lakini kwa muda wote wa miaka miwili ya mapenzi yetu alikuwa akinitenda mno, alinidanganya mengi, ilifika kipindi aliniletea dada wa ndani kumbe ni mke mwezangu, nilipochunguza nikagundua kwamba ana mke aliyekuwa akiishi Kimara na pia nilisikia tetesi za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki, Pauline Zongo, nilipomuuliza alikataa.”

Anasema anakumbuka maisha ya Mtunisi kama maigizo, hakuwahi kumwambia kama alikuwa na mke, lakini alipofanya uchunguzi wake akagundua kwamba alikuwa na mke Kimara, alipomfuatilia yule mwanamke akaja moto akiwa na gazeti lake lililoandikwa habari zangu kuhusu Mtunisi, lakini baada ya kumtuliza na kuzungumza, tukatambua kwamba mwanamume huyo alikuwa akituchezea bila kujijua.

“Mtunisi alikuwa ndani, alipotoka akanipiga kibao, akidai nimekwenda kumfanyia fujo, hapo akaongeza hasira, mimi na yule mwanamke wake tulimchangia tukampiga sana, hatasahau na mapenzi yakaishia hapo, kila mtu akawa na maisha yake sina cha kukumbuka, zaidi najutia kupoteza muda wangu kwake,’’ anaeleza Batuli.

Kuasili watoto
Akielezea maisha ya kuwa na watoto zaidi, anasema anatamani watoto zaidi lakini wa kike tena wawe mapacha.

“Napenda mtoto wa kike kwa kuwa nina watoto wawili wa kiume, nitazungumza na wataalamu wa masuala ya uzazi kama nitafanikiwa sawa lakini nikishindwa nitaasili mtoto wa kike,’’ anaeleza.

Chanzo:  Mtanzania Gazeti

KAJALA ATAMANI WATOTO MAPACHA

 http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/2523274/lowRes/876457/-/bd70tk/-/kajala_clip.jpg
Staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja ameweka wazi kuwa mipango yake ya kuzaa watoto iko palepale na kwamba safari hii angependelea kuzaa watoto mapacha.

Licha ya kwamba Kajala ana binti yake aitwae Paula, atahakikisha anamtafutia wadogo zake kwani hata yeye amekaa kwenye falimia ya watoto wengi na angependelea na yeye kuwa na familia kubwa. Kajala amebainisha kwamba hafikirii kupata mtoto na mume wake ambaye kwa sasa yuko gerezani bali anatafuta mwanaume mwenye malengo ya maisha na mwenye kujali familia.

Licha ya kuwa na mipango yote hiyo Kajala ameelezea ugumu anaoupata katika lengo lake la kuilea hiyo familia kwani hadi sasa binti yake Paula anakosa raha kutokana na skendo zinazotengenezwa dhidi yake.

Amesema hali hyo imekuwa inamnyima raha binti yake huyo hata anapokuwa shuleni kwani wenzake humnyooshea vidole kila wakati kutokana na taarifa ambazo alisema si sahihi kuhusu mama yake.
Chanzo: Bongomovie.com

AUNTY EZEKIEL AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE

aunt
Aunty Ezekiel.
Jana ilikuwa siku ya furaha kwa familia ya wasanii wawili Aunt Ezekiel ambaye ni m'bongo movie na dansa wa Diamond aitwaye Mose Iyobo baada ya kujaaliwa kupata mtoto wa kike.

Mtoto huyo amepewa jina la Cookie na Aunty alionesha furaha yake kwa kuandikwa kwenye ukurasa wa instagram ujumbe wa kumshukuru Mungu kwa kumfanikisha kujifungua salama.
antiiiii
Ujumbe wake uliendelea…
 
wajizaniao wao ni miungu watu Bac endelea kunyoosha mkono wako ktk paji la kiumbe wako ukiwa kama kinga nami niwe kivuli tuu juu yake Amen Whn Jesus Say Yes Nobody can Say wht!!!!!!!Wlcm Baby Cookie wlcm 2 da world KIBOKO YANG…
iyobo
Aunty Ezekiel akiwa na baba Mose Iyobo ambaye ndiye baba wa mtoto wake.
 Wakati huo huo, Diamond ambaye ni bosi wa baba wa mtoto Cookie, amewapongeza wazazi hao kwa kuandika hivi katika ukurasa wake wa instagram:
diamond