Tuesday, February 10, 2015

KILICHOAMULIWA NA FAMILI KUHUSU HATMA YA MTOTO WA MAREHEMU WHITNEY HOUSTON

Bobbi Kristina Brown, 21 - Mtoto wa marehemu Whitney Houston.
Zikiwa ni siku 10 tangu Bobbi Kristina apoteze fahamu na kuendelea kutumia mashine zinazomsaidia kupumua hadi sasa, imeelezwa hali yake bado haijabadilika tangu adondoke bafuni na kukimbizwa katika hospitali ya Emory University iliyopo Atlanta, Marekani.

Kwa mujibu wa familia ya Kristina na madaktari wamekubaliana kumwondolea mashine anayopumulia kesho ikiwa ni siku ambayo mama yake mzazi Whitney Houston alifariki dunia katika mazingira ya kudondoka bafuni kama mtoto wake.  Hii ni ishara kuwa mama na mtoto watakuwa wamekufa katika tarehe moja.
Baba mzazi wa Bobbi Kristina, Bobby Brown akitoka hospitali.
Madaktari wameonyesha kukata tamaa ya kurejesha tena maisha ya mtoto huyo na kuamua kuiachia familia juu ya hatma ya mtoto wao kuhusu kutoa mashine anayopumulia.