Thursday, March 15, 2012

MWANAMKE AMNYANYASA MWANAE KIJINSIA, DAR

Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni!!

Mwanamke huyo pichani mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akimfanyia vitendo vya usagaji mwanae wa kike wa kumzaa mwenye umri wa miaka 7 kwa kumwingiza uume wa bandia katika sehemu zake za siri, mbele na nyuma na kumharibu vibaya katika sehemu hizo.

Kwa maelezo ya mama huyo, huyo ndio mtoto pekee aliye nae na alimpata kwa kubakwa na mwanaume akiwa anasoma kidato cha kwanza ambapo hadi leo baba wa mtoto hajafahamika.  Imegundulika pia kuwa mama huyo amekuwa akiwafanyia hivyo hata watoto wengine.

Inasemekana kuwa mwanzoni mama huyo alipoulizwa hakushtuka kusikia kuwa mwanae kaharibika na alikataa kuwa sio yeye aliyemfanyia kitendo hicho mwanae. 

Baada ya kupewa kichapo na wananchi ndipo alianza kulia na kukubali kuwa ni yeye ndie aliyemfanyia hivyo mwanae na hajielewi ni kwanini anafanya hivyo.

Pia katika kutapatata mama huyo aliomba apelekwe jela au awekwe mahali peke yake asionane na mtu yoyote au auawe kwa sababu hajitambui kwa nini anafanya hivyo.

Taarifa ya unyanyasaji jinsia wa mtoto huyu ilirushwa leo katika kipindi cha Leo Tena - Hekaheka cha redio ya Clouds kinachorushwa kuanzia saa 5.15 asubuhi.

Kwa taarifa zaidi pitia katika address ifuatayo: